Watu Wasiojulikana | Jinsi Ya Kujikinga Na Kukabiliana Nao
Kitabu hiki bora kabisa kitakupatia mbinu mbalimbali za kujikinga dhidi ya Watu Wasiojulikana, sambamba na hatua za kuchukua endapo utabaini kuwa maisha yako yapo hatarini. Ni kitabu ambacho lazima uwe nacho katika kipindi hiki kilichogubikwa na janga la utekaji linalofanywa na Watu Wasiojulikana.
Kitabu kina sehemu mbili. Ya kwanza ni maelezo ya mwandishi kuhusu masahibu aliyopitia, na jinsi alivyoweza kukabiliana na jitihada mbalimbali zilizofanywa na Watu Wasiojulikana kwa lengo la kumdhuru.
Sehemu ya pili ni maelezo ya hatua kwa hatua endapo unataka tu kujilinda dhidi ya Watu Wasiojulikana au endapo unaona dalili/ umetishwa kuwa Watu Wasiojulikana wanakuwinda.